Dar es salaam. Baada ya mchezo wa Jana wa ngao ya jamii, uliomalizika kwa Yanga kushinda mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao simba, msemaji wa wekunde wa msimbazi Ahmed Ally ameandika maneno mazito kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Ahmed aliandika hivi;
"Maumivu ni makali sanaa๐ญ๐ญ
Hakuna anaeweza kujificha kwa kusema ni kawaida ya mpira, mateso hayapaswi kuwa kawaida
Ukweli ni kwamba tunapitia maumivu makali mnoo, kila mwana Simba leo anaugua kivyake
Poleni sana ndugu zangu hakuna neno la kufuta machungu yenu
Mlichokitegemea sicho mlichopata inaumiza sana, kila nikitazama macho ya Wana Simba naona uchungu na maumivu yaliyopitiliza, kiukweli mnateseka ndugu zangu ๐ญ
Tumeshapoteza, tutulie tuone tunaingiaje msimu mpya, Sio rahisi kusahau lakini tunapaswa kujisahaulisha maana ligi inaanza wiki ijayo ni muhimu zaidi kuanza vizuri
Panapovuja pameonekana tuwaachie wahusika wafanye maamuzi sahihi"
Poleni๐๐๐๐ญ๐ญ
0 Comments