OKWA AWAOMBA MSAMAHA MASHABIKI WA SIMBA

 Dar es salaam. Nyota mpya wa Simba aliyesajiliwa kutokea klabu ya Rivers United ya Nigeria, Nelson Okwa amewaomba msamaha mashabiki wa Simba Sc Baada ya kupoteza mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya Yanga.



Okwa alisema mashabiki walitegemea makubwa kwenye mchezo huo na waliwaamini wataibuka na ushindi lakini Mambo yalikwenda ndivyo sivyo.

"Tutarudi kwa nguvu kubwa katika mechi nyengine za mbele, hatupaswi kuongea zaidi kuhusu mchezo huu lakini ni vyema kufanya kweli uwanjani". Alisema Okwa.

Okwa aliingia kipindi Cha pili kuchukua nafasi ya winga Kibu Dennis na alipiga shuti lililolenga nguzo kwenye lango la yanga.

Post a Comment

0 Comments