Dar es salaam. Tangu aliposajiliwa na Yanga, Fiston Mayele ametimiza mwaka sasa akitokea Vita Club ya nchini Congo.
Mayele ameifungia Yanga jumla ya mabao 22 katika mechi zote alizocheza za mashindano yote.
Kiujumla Mayele amezifunga timu 13 ambazo ni Simba, Polisi, KMC, Geita Gold, Biashara, Coastal, Azam, Namungo, Kagera Sugar, Mbao, Mbeya Kwanza, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar.
Mayele amezifunga mabao matatu, Simba, Coastal Union na Biashara United kwa Mara zote alizocheza nao.
Timu ambazo Mayele hajawahi kuzifunga ni Mbeya City, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting pekee kwa msimu ulioisha.

0 Comments