Arusha. Kocha mkuu wa Yanga, Professor Nassredine Nabi amesema kuwa licha ya kuanza na ushindi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya NBC ila bado anahitaji kufanya maboresho makubwa.
Nabi amesema kuwa bado kikosi chake hakijapata muunganiko mzuri anaoutaka na hiyo inatokana na wachezaji wengi kuwa wazuri hivyo anahitaji muda wa kuwa na kikosi chake.
Yanga ambao kesho jioni watashuka dimbani kukipiga dhidi ya Coastal Union uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha kwasasa wanajiandaa na mchezo huo.
Mechi ya mwisho kwa wawili hao kukutana jijini hapo iliisha kwa sare ya 3-3 na Yanga kuibuka na ushindi kwenye penalty.

0 Comments