YANGA YA GSM YATAKA REKODI HII, KWENYE LIGI KUU YA NBC

 



Arusha. Klabu ya wananchi, Yanga SC leo leo wanashuka dimbani kukipiga dhidi ya wenyeji Polisi Tanzania uwanja wa Sheikh Amri Abeid majira ya saa 10:00 jioni, huku wakiisaka rekodi mpya.

Yanga ambao walimaliza ligi msimu uliopita bila kufungwa mchezo wowote sasa wanaanza msimu mwengine wa ligi ya NBC na kutaka kuandika rekodi mpya ya kutokufungwa Tena.

Msimu uliopita yanga ilicheza michezo 37 bila kufungwa, rekodi ambayo bado mechi moja kumfika Azam FC ambao walitimiza mechi 38 bila kufungwa.

Endapo yanga itashinda mechi yao dhidi ya Polisi leo na ile dhidi ya Coastal Union uwanja huo huo siku chache mbeleni wataandika rekodi mpya ya kutokufungwa mechi 39.

Kocha wa Yanga, Professor Nassredine Nabi ameuzungumzia mchezo huo na kusema hautakuwa mchezo rahisi kwao Kama wengi wanavyodhani kwasababu ya uwepo wa nyota wapya Kama Aziz Ki na Morrison ambao waliuwasha moto kwenye mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Simba.

"Polisi ni timu ngumu haijawahi kuwa mechi rahisi kila tunapokutana lakini tumejipanga kushinda ili kuanza ligi kwa nguvu na matokeo chanya" alisema Nabi. 

Post a Comment

0 Comments