Dar es salaam. Inaelezwa kuwa mabeki wa Kati wa Simba Sc, Henock Inonga Baka na Mohammed Quattara wapo matatani kutocheza tena pamoja kama wataendelea kuboronga Tena.
Hilo limezuka Mara baada ya Simba kupoteza mchezo wa ngao ya jamii dhidi ya mahasimu wao yanga, na kocha wa timu hiyo Maki Zoran amezungumzia pacha hiyo walioonyesha kuboronga kwenye mchezo huo.
"Wote hawakueleweka nani anamaliza tano, walionekana kucheza namba moja (namba nne) hivyo wakajikuta wanamsahau yule streka aliotufunga mabao mawili" alisema.
Zoran amewataja mabeki Erasto Nyoni, Kennedy Juma na Joash Achieng 'Onyango' kama mabeki mbadala ambao wataweza kuchukua nafasi ya mmojawapo Kama wataendelea kuboronga.

0 Comments