BAADA ya gazeti la Mwanaspoti kuweka wazi kushindwa kukamilika kwa usajili wa winga mpya wa Yanga Tuisila Kisinda, Shirikisho la soka nchini 'TFF' limetolea ufafanuzi sakata hilo.
BAADA ya gazeti la Mwanaspoti kuweka wazi kushindwa kukamilika kwa usajili wa winga mpya wa Yanga Tuisila Kisinda, Shirikisho la soka nchini 'TFF' limetolea ufafanuzi sakata hilo.
Mwanaspoti katika toleo lake la leo Septemba 5, 2022 limeeleza usajili wa Kisinda umekuwa na sintofahamu kutoka TFF baada ya Yanga kuandikiwa barua ya kuzuia kumtumia nyota huyo jambo lililowashtua mabosi wa Yanga lakini masaa matano baadae TFF imekuja na ufafanuzi.
Taarifa ya TFF kwa umma imefafanua namna ilivyofanya usajili wa kigeni hasa kwa klabu zinazowakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ikieleza kuwa usajili huo ulishapitishwa na Kamati ya Hadhi za Wachezaji wa TFF na kuoongeza;
"Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji katika mazingira maalumu ilishughulikia haraka usajili wa wachezaji hao wa kigeni ili wawahi usajili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu usajili wa wachezaji wa kigeni.
Wachezaji wote wa klabu hizo, Azam, Geita Gold, Simba na Yanga walishapewa leseni zao kwa ajili ya msimu wa 2022/2023 ambazo pia ndizo zimetumika kuwaaombea usajili kwaajili ya mashindano ya CAF.
Kwa mujibu wa kanuni ya 62 (1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12. Hivyo klabu kutaka au kujaribu kusajili wachezaji zaidi ya idadi hiyo ni kwenda kinyume na kanuni."
Kwa mujibu wa kanuni hiyo, huenda Kisinda asipate nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha Yanga kwani wachezaji 12 waliosajiliwa awali kabla yake ni Djigui Diarra, Djuma Shaban, Joyce Lomalisa, Yanick Bangala, Gael Bigirimana, Kharid Aucho, Jesus Moloko, Fiston Mayele, Stephene Aziz Ki, Benard Morrison, Lazarous Kambole na Herritier Makambo.
0 Comments