HAWA HAPA NYOTA WA SIMBA WASIOCHEZA MCHEZO WOWOTE WA LIGI MWAKA HUU.

 Dar es salaam. Klabu ya Simba SC mpaka sasa inaongoza ligi kuu Bara kwa idadi kubwa ya magoli na alama sita mkononi, wakiwa sawa na mahasimu wao yanga na Singida Big Stars.



Simba wameshinda michezo miwili nyumbani, huku mchezo wa kwanza wakiifunga Geita Gold mabao 3-0, na Kisha kuwafunga kagera 2-0 na kuwa timu isiyo ruhusu bao mpaka sasa kwenye ligi kuu.

Lakini pia wekundu hao wa msimbazi jumatano ya September, 07 itashuka kukipiga dhidi ya KMC uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam, ikiwa ni mchezo wa raundi ya tatu ligi ya NBC.

Kikosi cha Simba takribani wiki moja kilikuwa nchini Sudan walikoalikwa na klabu ya Al Hilal, wakifanikiwa kushinda mechi moja tu ule dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana wakishinda mabao 4-2 na kufungwa mchezo mmoja tu dhidi ya wenyeji Al Hilal bao 1-0.

Simba wamerejea leo nchini Tayar kwa mchezo wa ligi kuu jumatano dhidi ya KMC, huku wakitarajiwa kucheza na Arta ya akina Alex Song na Solomon Kalou,mechi ya kirafiki.

Hapa tunakuletea nyota wa Simba wapya na wale wa zamani ambao hawajacheza mchezo wowote wa ligi kuu mpaka sasa.

Nyota hao ni hawa hapa wageni na wazawa.

Nasoro Kapama

Amejiunga na Simba SC mwaka huu akitokea Kagera Sugar Kama mchezaji huru. Kapama anaingia kwenye orodha ya nyota wa Simba wasio onja radha ya ligi kuu msimu huu kutokana na kutopewa nafasi.

Kapama licha ya kutocheza mchezo wowote wa ligi kuu, Lakini amecheza mechi mbili mfululizo za kirafiki ambazo Simba wamecheza kule nchini Sudan walipoalikwa na Al Hilal.

Kocha wa Simba, Maki Zoran alinukuliwa akisifia kiwango alichoonyesha nyota huyo kwenye mechi hizo huku akisema ana mapungufu madogo tu ambayo yanarekebishika.

Victor Akpan

Simba ilitoa kiasi cha Sh. 100 milioni kupata saini ya nyota huyu kutoka Nigeria aliyekuwa na msimu Bora msimu uliopita akiwa na Wagosi wa Kaya, Coastal Union.

Akpan hajacheza mchezo wowote wa ligi kuu Lakini mpaka sasa amecheza mechi mbili akiwa na Simba zote zikiwa za kirafiki za kimataifa moja ikiwa ni ule wa Simba day dhidi ya St. George ya Ethiopia na ule wa Sudan dhidi ya Asante Kotoko ya Ghana.



Zoran alinukuliwa akisema Akpan ni mzito akiwa uwanjani ndio Mana hamtumii na yeye anahitaji  viungo wenye kasi.

Joash Onyango Achieng

Nyota wa kimataifa wa Kenya, Joash Onyango alikuwa na msimu Bora toka alipojiunga na Simba Lakini furaha yake ilikufa gafla Mara tuu baada ya ujio wa beki wa kimataifa wa Burkina Fasso Mohammed Quattara.

Onyango mpaka sasa hajacheza mchezo wowote ule akiwa na Simba huku akidai kusepa klabuni hapo kabla ya mwenyekiti wa klabu hiyo Try Again kuyamaliza na nyota huyo ili aendelee kusalia klabuni hapo kwani wanamuhitaji bado.

Onyango ambae ameshawahi kukipiga Gor Mahia ya nchini kwao Kenya, mapema mwisho wa mwezi huu alihusishwa kutua Singida Big Stars Lakini beki huyo kisiki anayesifika kwa kukaba amekubali yaishe na atajiunga na kikosi Tayari kwa mechi zijazo za ligi na zile za kimataifa.

Kennedy Juma

Beki huyu mzawa nae anaingia kwenye orodha akiwa hajacheza mchezo wowote ule wa ligi mpaka sasa.

Kennedy kwasasa yupo kwenye kikosi Cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambao wanajiandaa kwaajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Uganda kufuzu Chan.

Stars ilikubali kichapo Cha goli 0-1 bila nyumbani hivyo Wana deni la kulipa pale kwenye ardhi ya Mseveni.

John Raphael Bocco

Nahodha wa Simba nae mpaka hajacheza mchezo wowote ule wa Simba mpaka sasa na ripoti zinasema majeraha ndio sababu.

Bocco ambae aliibuka mfungaji bora wa ligi kuu mwaka juzi msimu wa 2020/21 hakuwa kwenye msimu mzuri mwaka jana.

Bocco kwasasa amejumuishwa kwenye kikosi Cha taifa stars tayari kwa mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda the Cranes jumamosi hii.

Nyota wengine wa Simba WASIOCHEZA mchezo wowote ule wa  ligi kuu mpaka sasa ni pamoja na Berno David Kakolanya, Ally Salim, Jimyson Mwanuke, na Gadiel Michael Mmbaga Kamagi.

Story na Jackson Ngowo.


Post a Comment

0 Comments