Dar es salaam. Usiku wa Jana majira ya saa 5:59 mabingwa watetezi wa ligi ya NBC, Yanga SC walimtambulisha mchezaji wao mpya ikiwa bado dakika moja tu dirisha lifungwe.
Yanga walimtambulisha Tuisila Kisinda, 22, Kama mchezaji wao mpya ambae amerejea tena viunga hivyo vya Jangwani akitokea RS Berkane aliojiunga nao mwaka 2021.
Kisinda amewatumikia Berkane kwa mwaka mmoja tu na kufanikiwa kubeba kombe la shirikisho barani Afrika mbele ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.
Mpaka sasa maswali ni mengi kwa mashabiki wa Yanga wakijiuliza wachezaji gani wa kigeni watasepa baada ya ujio wa nyota huyo wa kongo kwani yanga wamefikisha idadi ya nyota 14 wakigeni.
Iko hivi Lazalous Kambole amejiunga na yanga mwaka huu akitokea Kaizer Chiefs Lakini mpaka sasa hajacheza mchezo wowote ule akiwa na yanga, inasemekana ni majeruhi wa muda mrefu, hivyo basi ujio wa Kisinda tayari ni kwaajili ya kuchukua nafasi ya nyota huyo Mzambia ambaye yanga wanaonekana kutaka kumtema mapema kabisa ili kupunguza idadi ya nyota wa kigeni klabuni hapo.
Nyota wengine wanaopigiwa chapuo kusepa klabuni hapo ni pamoja na Yacouba Sogne, Heritier Makambo na Jesus Moloko.
Uwezekano wa Moloko kusepa Jangwani ni mdgo kutokana na kocha kuonekana kuwa na mipango nae.
Yanga imeanza vizuri msimu mpya wa ligi kuu, huku macho ya wengi yakitamani kuona wanafanya vizuri kimataifa kutokana na usajili waliofanya msimu huu.
0 Comments