Dar es salaam. Wananchi kwa sasa wanachekelea mpunga mrefu walioupata Mara baada ya kuwafunga Simba mabao 2-1 kwenye ngao ya jamii siku ya jumamosi.
Yanga waliahidiwa kupewa Sh.milioni 200 endapo wangeifunga Simba.
Yanga walifanya ivyo ndani ya dakika 45 za kipindi Cha pili tu, kwa mabao ya King Mayele.
Pesa hizo waliahidiwa na GSM ambao ni mdhamini wao wa jezi Lakini pia wanajitoa kwenye kukamilisha sajili mbalimbali kwenye klabu hiyo.
Kwa sasa yanga wapo Arusha kwaajili ya mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania wakianza ugenini, uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mara baada ya kukipiga na Polisi yanga watabaki Arusha kwaajili ya kukipiga dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambao uwanja wao upo kwenye marekebisho makubwa.

0 Comments