NGAO YA JAMII KUHUSISHA TIMU NNE MSIMU UJAO

BODI ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetangaza kuanzisha Shindano jipya ambalo litakuwa maalumu kwaajili ya Ufunguzi wa Ligi (Ngao ya Jamii) litakaloshirikisha timu zilizoshika nafasi ya tatu za juu kwenye Msimamo wa Ligi na Timu Bingwa wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).



Kwenye Shindano hilo,Endapo Bingwa wa Ligi Kuu Ndiye atakuwa Bingwa wa Kombe la Shirikisho pia basi yule aliyeshika nafasi ya nne kwenye Ligi Kuu atashiriki Shindano hilo.



Pia Bodi ya Ligi imetangaza Kuwa Sherehe za Utoaji wa Tuzo utafanyika siku tatu mara Baada ya Fainali ya Kombe la Shirikisho kuchezwa.

Post a Comment

0 Comments